Stori: Imelda Mtema
MWANAMITINDO maarafu Bongo, Belina Mgeni amejifungua mtoto wa kike.
Mtoto wa Belina.
Mrembo huyo alijifungua juzikati katika Hospitali ya TMJ, iliyopo
Mikocheni, jijini Dar es Salaam ambapo mwanamitindo huyo hakusita
kuanika furaha yake mbele ya paparazi wetu kisha akatangaza jina la
kichanga hicho, Naila.“Kiukweli siku zote ukimuomba Mungu unafanikiwa kwani nilikuwa naomba sana nipate mtoto wa kike na kweli imekuwa, namshukuru Mungu jamani,” alisema Belina pasipo kumuanika baba wa mtoto huyo.