Nisha alipokuwa anaumwa |
MSANII nyota wa filamu Tanzania, Salma Jabu maarufu
kama Nisha yamemkuta makubwa baada ya habari kuvuja kuwa kumbe sababu ya kuumwa
hadi kuzidiwa kitandani, ilitoka na kuchoropoa mimba changa aliyokuwa nayo.
Gazeti la Maskani Bongo lilitonywa na mtu wa karibu wa msanii huyo ambaye yupo ndani ya familia hiyo baada ya kusambaa kwa habari kuwa Nisha aliugua gonjwa la ajabu ghafla katika mitandao ya kijamii na magazeti pendwa..