Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.
William Mgimwa kwa sasa unaagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar
kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa maziko. Dk. Mgimwa
alifariki dunia Januari 1 mwaka huu akiwa Hospitali ya Mediclinic Kloff
nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.