Askari
Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye
ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako
alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya
madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa
mwingine mkoani Morogoro.Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.