STAA wa muziki wa Pop, Justin Bieber atalipa faini ya dola 80,900,
kuhudhuria kozi ya wiki 12 kudhibiti hasira zake na siku tano za
kushiriki kazi za kijamii kwa kosa la kumrushia mayai jirani yake.
Staa huyo pia atatakiwa kukaa umbali wa yadi 100 kutoka kwa familia hiyo huku akiwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili.
Bieber alinaswa na jirani yake akirusha mayai katika nyumba yake
mwezi Januari na hukumu yake imetoewa jana huko Los Angeles na
kuhudhuriwa na mwanasheria wake, Shawn Holley.