Polisi
Kusini mwa India wamesajili kesi ya ubakaji ambapo inaarifiwa mtoto wa
shule mwenye umri wa miaka 6 alibakwa na wafanyakazi wawili wa shule
moja maarufu mjini Bangaloer.
Kisa
hicho kinaarifiwa kutokea wiki mbili zilizopita. Mtoto huyo alibakwa na
mlinzi pamoja na mwalimu, lakini kwa sababu ya kuwepo walinzi wengi
katika shule hiyo, polisi bado wanachukua muda kuchunguza mlinzi
aliyehusika.
Polisi
wanasema kuwa mtoto huyo alibakwa tarehe mbili Julai , lakini wazazi
wake waligundua hilo siku chache zilizopita baada ya mtoto huyo
kulalamika kuumwa na tumbo na kupelekwa hospitalini.
Wakati huo mamia ya wazazi wameandamana nje ya shule wakivunja milango na kupiga mayowe kulaani tukio hilo.
Polisi tayari wamesajili kesi hiyo , lakini bado hawajamkamata mtu yeyote.
Mwandishi wa BBC Andrew North mjini Delhi anasema kuwa tukio hilo ni la hivi karibuni kugonga vichwa vya habari nchini India.
Waziri
mkuu Narendra Modi, ameahidi kupambana vilivyo na visa vya ubakaji, na
udhalilishaji wa kijinsia , lakini unyanyasaji wa wanawake bado ni
tatizo kubwa sana nchini humo.
Huku
taarifa ya kubakwa kwa mtoto huyo zikijitokeza tu, mamia ya wazazi
walikusanyika nje ya shule hiyo na kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya
wasimamizi wa shule.
Mnamo
siku ya Alhamisi mwenyekiti wa shule Rustom Kerawala alizungumza na
wazazi ambapo aliomba msamaha na kuahidi kushirikiana na polisi katika
uchunguzi.