Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.
Kufuatia
tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu
mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika
eneo la Mtaa wa Congo.
Akithibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally
Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na
atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa
kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku
akijua ni kosa kisheria.
Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo
Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo