Kijana ambae ni kibaka na
ahakufahamika jina lake akisurubiwa na wana usalam baada ya kuchana na
wembe Askari Polisi aliyekuwa uwanjani kwenye shoo ya Open Mic
iliyofanyika kwenye viwanja vya Temeke Mwembe Yanga mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Kijana aliomba ardhi ipasuke kwa kipigo kikali ambacho hakika bila na nguvu za giza watu wangesimulian Na Livingstone Mkoi
Kijana asiyejulikana jina lake
hivi karibuni alionja joto ya jiwe kwa baada ya kuchezea kipigo cha mbwa
mwizi toka kwa wanausalama waliokuwa uwanjani kufuatia kumjeruhi Askari
Polisi kwa kumchana na wembe mgongoni wakati askari huyo akimkamata
mmoja wa vibaka hao.
Hata hivyo kutokana na wingi wa
vibaka ambao ni wazoefu wa eneo hilo walipambana vya kutosha na wana
usalama.Hata hivyo wakati wanausalama hao wakijaribu kumkamata mmoja wa
vibaka waliokuwa wanapora wananchi ndipo kibaka mmoja anaeonekana
pichani alipojitoa muhanga na kumchana kwa wembe Polisi.
Baada ya tukio hilo kijana huyo
alikamatwa na kuanza kuchezea kichapo cha nguvu,huku polisi huyo
akikimbizwa Hospitali kutibiwa.