Jemma Benjamin |
Wengi tunaamini kuwa mtu hupata mshtuko baada ya kupewa taarifa mbaya ama kushtuliwa kutokana na uoga wa kukwepa ajali. Lakini msichana Jemma Benjamini (18) alifariki kutokana na hisia alizopata baada ya kukiss kwa mara ya kwanza maishani mwake (First Kiss), April, 2009.
Kwa mujibu wa mtandao wa telegraph wa Uingereza, Msichana
huyo muingereza ambae alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, alipoteza maisha baada
ya kupigwa busu na mwanafunzi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Daniel Ross
(21) nyumbani kwao na kijana huyo baada ya kutoka kwenye mtoko wa usiku kama
marafiki.
Lakini katika mishemishe za kukaa pamoja kwa dakika kadhaa
kwenye sofa wakibadilishana maelezo kadhaa walijikuta wakikiss taratibu, muda
mfupi baada ya kiss hiyo Daniel alimuona mwenzake analegea taratibu huku macho
yake yakiishiwa nguvu na kisha kutulia kabisa.
Hali hiyo ilianza kumtisha kijana huyo ambae anasema
hawakuwahi kuwa na mahusiano ya mapenzi kabla, na hiyo ilitokea tu wakajikuta
wanakiss.
“Haikuwa mahusiano ya mapenzi lakini tulikuwa tukikutana
mara kadhaa kwa wiki, tulikuwa tunaelekea bar kupata chakula na tukarudi
nyumbani kwa kuwa nilikuwa nimesahau credit card, tulikuwa tunaongea na
tukajikuta tunakiss.
“Tulienda jikoni na baadae kwenye chumba cha kupumzika na
Jema akakaa kwenye sofa,nikaanza kuona macho yake yanaanza kulegea ghafla
kushuka, na mdomoni akaanza kutoa vijipovu vya mate kabla hajaanguka.”
Baada ya hapo alimpigia simu mama yake kisha akapiga simu
kuomba msaada zaidi wa matibabu na ambulance ilifika na kumkimbiza hospital
ambapo aligundulika kuwa tayari alikuwa ameshafariki.