Mwili wa jamaa huyo ukiwa katika difenda.
Wananchi wakiwa wamekusanyika katika gesti ya Uroda alipofia jamaa huyo.
Jamaa mmoja ambaye hakujulikana
jina lake leo amekutwa amekufa katika gesti bubu iitwayo Uroda iliyopo
Manzese Midizini jijini Dar. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la
tukio ni kwamba marehemu alikuwa na mpenzi wake ambaye waliingia wote
katika gesti hiyo lakini alikutwa jamaa peke yake. Mwili wa marehemu
umepelekwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.