BAADA ya watanzania kumwandama
Ommy Dimpoz kutokana na tusi alomtukana marehemu Albert Mangwea, msanii
huyo ameamua kuwapigia magoti watanzania na kuwasihi
wamsamehe.
Hali hiyo imekuuja baada ya watu
mbalimbali kutangaza kumsaka Ommy kwa lengo la kumwadabisha kwa
kumpa kichapo kikali.
Miongoni mwa watu hao ni TID ambaye
jana kupitia ukurasa wake wa facebook ametangaza vita dhiti ya
Ommy Dimpoz.
Hii ni post ya Ommy ambayo ameitoa akiomba asamehewe kwa kauli zake na matusi aliyoyatoa kwa marehemu Ngwea.
Samahani tena sana na sitawacha kuomba msamaha, nimekubali
makosa na hivi sasa naelekea nyumbani kwao kuomba msamaha kwa familia na nitue
kwa vituo vya radio kuomba msamaha kwa wabongo na wote niliowaudhi. Samahani
sana na nakubali mimi si mtu bila nyinyi na sikuongea kuhusu legend Ngweir kwa
ila mbaya. One love