NI
siku ya furaha kwa Kanye West! Kim Kardashian amejifungua mtoto wa kike
Jumamosi asubuhi katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center, Los
Angeles, mtandao wa OMG umethibitisha.
Inasemekana
Kardashian, 32, alikuwa na West pembeni mwake wakati wa kujifungua,
kumkaribisha duniani binti yao mwezi mmoja kabla ya muda uliotarajiwa.
Tarehe halisi ya kujifungua ilitazamiwa kuwa Julai 11.
"Kim
aliugua Ijumaa usiku na hatimaye kupata mtoto mapema," chanzo cha
hospitali kimeileza Us Weekly. “Inafurahisha, wote katika hali nzuri!"
Kanye
West, 36, na Kim - wote wawili wakiwa ndo mara ya kwanza kuwa wazazi,
wamekuwa wapenzi tangu Aprili 2012. Desemba 30, 2012, West alitangaza
kwamba mpenzi wake alikuwa na mimba wakati wa tamasha lake Atlantic
City.
"Simamisha
muziki na wote mpige kelele kwa mama kijacho," alisema West jukwaani
akionyesha kidole kwa Kim ambaye alikuwa mmoja wa watazamaji.