M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitaliMsanii
M2 the P aliyekutwa mahuhuti pamoja na Ngwair ambaye alifariki,
anaendelea vizuri kiafya na ameshatoka hospitali. Mpaka sasa M To The P
hajui kama Mangwea amefariki na anadhani mwenzake ametangulia kwenda Dar
es Salaam.
“Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad”- Jestina George Kwa mujibu wa Jestina George, Magie amekuwa karibu sana na M2 The P na alikua karibu na marehemu Albert “Ngwair” Mangwea kwa muda waliokuwa Africa Kusini. kama inavyoonekana pichani, leo Magie alienda kumcheki M2 The P, kumpa moyo na kumchangamsha. Alipo fika alimkuta M2 The P amejawa na mawazo huku kikombe chake cha chai kiko mezani ikabidii aanze kumtania tania angalau aondokane na mawazo. Bado anamuuliza rafiki yake kipenzi Mangwea maana hajui yaliyo mfika. Tuendelee kumuombea M2 The P maana ana mtihani mkubwa mbele yake akija kujua ukweli, na ni Mungu pekee ndo ataweza kumsaidia