
HUU NDIO UKWELI KUHUSIANA NA UJUMBE HUU ULIOSAMBAA:
Jana jioni kuna meseji zilikuwa zikitembea zikisema kuwa Prod Majani amepigana na mtangazaji kutoka Clouds FM anajulikana kwa jina la Adam Mchomvu maeneo ya Learders Club wakati sio kweli kabisa. P-Funk yeye alikuwa bize na kamati na hadi uvumi huo unatokea Adam alikuwa hayupo kwenye eneo la tukio kabisa. Adam yeye alitokea majira ya jioni na kushangaa stori hizo, walipigwa picha hiyo ya pamoja wakiwa katika hali ya kawaida wala hakuna ugomvi.
