KIONGOZI wa
Kanisa la Roman Katoliki Duniani Papa Francis Jorge Mario ameshindwa kuonyesha
msimamo wake kwa mara nyingine kuhusu ndoa za jinsia moja.
Mdadisimambo Limenasa kauli ya Papa Francis
kutangaza nia yake ya kufanya kazi pamoja na watu wenye ndoa za jinsi moja ili
kuwasaidia katika maisha ya ndoa kupitia mitandao mbalimbali Duniani.
Kitendo cha
Kiongozi huyo mkubwa wa dini Duniani kutangaza nia yake ya kushirikiana na watu
wenye ndoa za jinsia moja imetafasiriwa tofauti huku watu wakishindwa kujua msimamo
wake kama anaweza kuruhusu ndoa hizo katika Kanisa lake ama ataendelea
kuzipinga.
Akizungumza na
Askofu wa Canterbury Justin Welby wa Kanisa la Anglikana wakati wa mazungumzo
yao katika makazi ya Papa huyo mjini Vatican alisema kwamba anampango wa kuwasaidia
wanandoa hao.
Hii ni mara ya
pili kwa Papa huyo kutoa kauli ambayo inazua utata kuhusu msimamo wake, mara ya
kwanza Papa Francis alisema kwamba watu wenye ndoa za jinsia moja wanastahili
kuishi katika jamii.
Papa Francis
alitoa kauli hiyo mara ya kwanza alipoulizwa swali na Waandishi wa Habari mara
baada ya kutangazwa kuwa Kiongozi wa Kanisa hilo lenye nguvu Duniani kuhusu
ndoa za jinsia moja.
Akijibu swali
hilo Papa Francis alisema kwamba, watu wenye ndoa za jinsia moja hususan
mashoga ni watu kama watu wengine na kwamba wanastahili kuishi katika jamii.
Papa Francis
alisema, watu hao wanapaswa kuwekwa karibu na Mwenyezi Mungu ili watubu na
kumtumia Mungu.
Papa Francis
ambaye alikuwa akipinga ndoa za jinsia moja tangu alipokuwa nchini wake
Argentina, alikutana na Askofu Welby ambaye hivi karibuni alitangaza nia yake
nchini Uingereza ya kusajiri taasisi itakayoshugulikia na ndoa za jinsia moja.
Katika
mazungumzo yake na Askofu Welby, Papa Francis alisema “Nina amini kwamba
tutashirikiana katika kutangaza maisha ya roho mtakatifu, na kuzipa uwezo
familia zilizopatikana ndani ya ndoa.