Kuna wakati mtu anaweza kuweka hadharani siri yake kwa nia njema ya kuokoa maisha ya watu wengine watokana na ushuhuda wake, na hii ni kwa kuwa watu wengi huwa wagumu wa kubadilika hadi waone mfano hai ama mtu aliyeathirika kutokana na tabia flani akitoa ushahidi.
Muigizaji mkongwe
mwenye umri wa miaka 68 Mmarekani Michael Douglas ameweka wazi kuwa tatizo lake
la kansa ya koo lilisababishwa na tabia yake ya kufanya mapenzi mdomoni(oral **ex)
Nguli huyo wa filamu alifunguka alipofanyiwa mahojiano na
gazeti la The Guardian la marekani ambapo alikanusha tetesi ambazo wengi
walikuwa wanaziamini kuwa uvutaji wa sigara na ulevi ndio uliosababisha yeye
kupata kansa ya koo.
Alisema ugonjwa alionao umetokana na maambukizi ya virusi
vinavyojulikana kama Human papolloma Virus (HPV) ambavyo vinasababisha magonjwa
ya zinaa.
Angalizo:
Tulikuwa tunasubiri mfano, na huu ni mfano hai unaothibitisha kuwa penzi la mdomoni na kunyonyana nyeti zetu ni hatari kiafya kwa kuwa husababisha kansa ya koo ....
Kuna njia nyingi za kuandaana kabla ya tendo.Hivyo si lazima tukatumia mdomo