Search in This Blog

UGOMVI WA BABA NA MAMA WASABABISHA KIFO CHA MTOTO KWA RISASI

KUSHOTO: Lisa Marie Lesyshen KATIKATI: Asher. KULIA: Michael Kirlan.
Mama wa mvulana wa miaka tisa alimpiga risasi mtoto huyo mara tano katika nyumba aliyokuwa akichangia na baba wa mtoto huyo huko Steamboat Springs, Colorado kisha akajigeuzia mwenyewe mtutu wa bunduki, kwa mujibu wa uchunguzi wa awali.
Lisa Marie Lesyshen alifyatua risasi na kumuua mtoto wake Asher, na kuacha kijikaratasi chenye ujumbe chini ya kitanda cha mtoto huyo akisema wa kulaumiwa ni baba wa mtoto huyo, Michael Kirlan kutokana na hatua yake hiyo.
Mume wake aliamshwa na vishindo vya risasi na kupiga simu polisi huku mama huyo akimtaka baba huyo kupokea bunduki hiyo na kumuua. Alinusurika.
"Kumbuka unahusika kwa kilichotokea hapa na wewe ni mtu uliyesababisha," aliandika, akisaini ujumbe huo, 'Lisa na Asher'.
Kwa mujibu wa taarifa, baba wa mtoto huyo alikuwa amelala katika nyumba hiyo wakati mauaji hayo yakifanyika na kuamka kufuatia mlio wa risasi majira ya Saa 9 usiku wa manane.
Ripoti za polisi zinasema wanandoa hao walikuwa wametengana na kulala katika vyumba tofauti wakati wa mauaji hayo.
Nyaraka za mahakama zilizowasilishwa Ijumaa zinasema Lisa Marie Lesyshen aliingia chumbani kwa mtoto wake na kumpiga risasi mvulana huyo mara tano kichwani, mguuni na kifuani. Nyaraka hizo zinasema mtoto huyo alikuwa amelala wakati akifyatuliwa risasi hizo.
Michael kirlan aliieleza polisi alikimbilia chumbani na kumuona Lisa akitoka chumbani kwa mtoto huyo na kuelekea chumbani kwake, akifuatiwa na milio miwili ya bunduki.
Kirlan alipiga simu polisi saa za mapema asubuhi ya Jumatano akisema mtoto wake amepigwa risasi na kwamba Lisa alikuwa na bunduki na alimtaka yeye amuue.
Maofisa walifika nyumbani hapo na kukuta Lisa akiwa amejeruhiwa na mtoto huyo wa miaka minane akiwa amefariki dunia.
Risiti zilizopatikana ntumbani hapo zinaonesha kwamba Lisa alinunua bastola aliyotumia kwa mauaji hayo ya mtoto wake siku mbili kabla ya tukio. Mfanyakazi aliyeuza bunduki hiyo alilazimika kumuonesha jinsi ya kujaza risasi.
Mfanyakazi huyo alieleza kwamba Lisa alisema anataka bunduki kwa ajili ya ulinzi wake binafsi sababu mumewe alikuwa nje ya mji, na alihitaji maelekezo ya jinsi ya kuitumia.
Lisa amekamatwa huku akisubiria kufunguliwa mashitaka ya mauaji, udhalilishaji mtoto uliosababisha kifo chake na vurugu nyumbani.
Nyaraka za mahakama zinasema kwamba Lisa amekiri mbele ya maofisa wa polisi kwenye Zahanati ya Kituo cha Afya cha Denver ambako amekuwa akitibiwa majeraha yake. Ameendelea kuwa chini ya ulinzi hospitalini hapo. Haijafahamika lini atapata nafuu ya kutosha kuruhusiwa kutoka hapo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger