Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema
Rais huyo, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa
ajili ya ziara ya siku tatu hadi Julai 3 mwaka huu ili
kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja na nchi
za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali
wakiwamo wafanyabiashara.