MAJERUHI WAKIWA HOSPITALI
Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa
kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA
katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga
kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.
Waliojeruhiwa
wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya
watu waliojitolea wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali
hizo kutoa huduma ya kwanza.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo. Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.