|
Dada anaetuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya. |
Akizungumza
na Gazeti la Mwananchi jana Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Wizara ya
Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mkubwa Ali, alikiri kukamatwa kwa
watu hao (majina yanahifadhiwa) ambao mmoja ni mkazi wa Ilala na
mwingine wa Magomeni jijini Dar es Salaam. “Taarifa tulizonazo zilizo
rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa sasa ni kukamatwa kwa
Watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha heroin kuelekea Bara la Asia
na walikamatwa nchini Misri wiki mbili zilizopita.”
“Tumewasiliana
na balozi wetu nchini Misri amesema hana taarifa za kuhukumiwa
kunyongwa kwa watuhumiwa hao, isipokuwa wameshasomewa shtaka lao la
awali. Wapo rumande kwa sasa kwani kesi hiyo imetajwa mara moja tu.
Balozi amekiri kushikiliwa kwa watuhumiwa hao wakiwa na dawa
zinazoaminiwa ni za kulevya,” alisema.
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa polisi na wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Video
inayomwonyesha mmoja akikaguliwa na maofisa wa polisi wa nchini Misri
na kukutwa na dawa hizo, ilisambaa siku nne zilizopita katika mitandao
mbalimbali ya kijamii.,
Kwa
mujibu wa sheria za Misri kama ilivyo kwa nchi za Bara la Asia, mtu
akikamatwa na dawa za kulevya hukumu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Kutokana na sheria za nchi hiyo, tangu kukamatwa na Watanzania habari
zimeenea kuwa huenda wakanyongwa.
Habari
za uhakika kutoka kwa ndugu wa karibu wa mtuhumiwa huyo, zilidai kuwa
walikuwa hawafahamu kuwa alikuwa anajihusisha na dawa za kulevya.
“Huyu ni ndugu yangu kabisa lakini nilikuwa sijui kama anafanya mambo kama hayo’’ alisema.
kama atanyongwa ni pigo kubwa kwetu,” alisema mmoja wa ndugu wa Sharifa ambaye hakupenda kutaja jina lake
Alisema
miaka mitatu iliyopita ndugu yao wa kike mwenye mtoto mmoja alikuwa
akifanya kazi katika Shirika la Nivea na alikuwa hana tabia mbaya.