AL SHABAB WALIOJITOKEZA HADHARANI NA KUSEMA NDIO WALIOSHAMBULIA KENYA HII LEO
Duka la kifahari lililoshambuliwa la Westgate katika mtaa wa Westlands Nairobi
Kundi la wanamgambo wa kiisilamu la Al shabaab nchini Somalia limedai kutekeleza mauaji ya watu zaidi ya thelathini nchini Kenya kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya ( Citizen TV) na pia kupitia kwa ukurasa wake wa Twitter...Shirika la habari la Reuters pia limesema kuwa Al Shabaab linasema kwamba Kenya ilipuuza mara kwa mara vitisho vya kundi hilo kuishambulia (Taarifa zaidi zinakujia). Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja amekatawa. Mshukiwa huyo amejeruhiwa na anapokea matibabu hospitalini.