Search in This Blog

BABA MZAZI WA WEMA HALI YAKE NI TETE



Maskini! Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa mkubwa wa filamu, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu yupo kitandani akiwa amepooza upande mmoja wa mwili wake.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mwishoni mwa wiki iliyopita aliiwakilisha serikali kwenda kumjulia hali mzee huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar na balozi katika nchi mbalimbali ambaye yupo nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar.
Katika hali ya kusikitisha, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu, aliliambia gazeti hili ambalo lilikuwa limeongozana na Nchimbi kuwa, mume wake alipatwa na ugonjwa huo akiwa kazini Zanzibar, ingawa kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na kisukari.
Alisema baada ya kupata taarifa za ugonjwa huo, familia ilipanda ndege kutoka Dar kuelekea Zanzibar ambako walimchukua na kumpeleka Hospitali ya TMJ ya jijini Dar, alikolazwa kwa muda wa wiki tatu kabla ya kuruhusiwa.
“Ingawa bado amepooza, lakini kwa sasa hali yake ni afadhali kuliko alivyokuwa mara ya kwanza,” alisema mama huyo aliyedai kuwa mumewe ni mgonjwa kwa mwezi mmoja sasa na kwa kipindi chote hicho, amekuwa akifanyiwa kila kitu.

CREDIT: GPL
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger