Picha iliyotolewa na mtandao wa
habari wa upinzani wa Syria, Shaam News Agency, inaonesha miili ya
watoto na watu wazima ikiwa imelala ardhini baada ya mashambulizi
yanayoshukiwa kuwa sumu siku ya tarehe 21 Agosti yaliyofanywa na
wanajeshi wanaounga mkono serikali mashariki mwa Ghouta, kwenye viunga
vya Damascus. (AFP/Shaam News Agency).
KATIBU mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon ameliarifu baraza la usalama jana jumatatu juu ya kile wakag
uzi wa silaha za kemikali walichogundua baada ya kufanya uchunguzi huko Syria.
Timu hiyo ilichukua sampuli ya mchanga kutoka kwenye mitaa ya Damascus na sampuli za damu kutoka kwa raia waathirika wa mashambulizi ya gesi ya sumu mwezi uliopita.
Kazi yao ilikuwa si kuangalia nani wa kulaumiwa lakini kuthibitisha shambulizi kutokea. Lakini Marekani inasema hakuna shaka yeyote kwamba jeshi la, Bashar Al Assad limehusika. http://www.voaswahili.com.

VIDEO: