BATULI:NAMUOGOPA MAMA KANUMBA ..NIKIMUONA HATA KUMSALIMIA SIWEZI
Staa anayesongesha maisha yake Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema akimuona mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa anaogopa hata kumsalimia kwa madai hukumbuka mambo mengi ya marehemu.
Akimwaga mawili matatu mbele ya kinasa sauti chetu, maeneo ya Kinondoni, jijini Dar, Batuli ambaye aliibuliwa na marehemu Kanumba kwenye filamu ya Fake Smile, alisema kamwe hawezi kuondoa uwepo wa marehemu katika ubongo wake na ndiyo maana anaogopa hata kumsalimia mama Kanumba.
“Ukweli ni kwamba bado sijawa na ujasiri wa kumkabili mama huyo, huwa nakumbuka mambo mengi sana kila nikimuona, naishia kumkimbia tu, hata pale Kariakoo juzikati niliogopa kabisa kumsalimia kwani ningeishia kulia mbele ya umati,” alisema Batuli.