Mwimbaji wa nyimbo za Injili Jijini Nairobi,Kenya,George Barasa maarufu
kama Joji Baro amejiatangaza kuwa yeye ni shoga.Mwimbaji huyo mwenye
umri wa miaka 22 akizungumza na mtandao mmoja wa nchini humo alisema
kuwa alizaliwa Jijini Nairobi na baadaye kuhamia Bungoma miaka michache
baadaye.
Aidha ameongeza kuwa pamoja ya kuwa ni shoga pia ameathirika na ugonjwa
hatari wa Ukimwi pia ni mwanaharakati wa kutetea Haki za Mashoga na
Wasagaji na wana zaidi ya wanachama 2,800,Ambao wote ni mashoga na
wasagaji ambapo vijana idadi yao 15 na watu wazima ni 68.
Alisema kuwa aliamua kuhamia Mjini EMBAKASI BAADA YA FAMILIA yake kumtenga alipojuliakana anajihusisha na vitendo hivyo.
Alipokuwa anasoma shule ya Mtakatifu Paulo Miluki High School ndipo
alipoanza kujifunza vitendo hivyo vya ushoga na kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki.
Machi 11, 2012 , Madaktari walimpima na kugundulika kuwa ni mwathirika
wa VVU / UKIMWI na kwamba amedai kuwa kwenye muziki wa INJILI amekuwa
akipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanamuziki mwenzake wa muziki huo.
Anasema amechoka kuhukumiwa na kuonewa huku akinyanyapaliwa na watu wengine baada ya kugundulika kuwa nafanya vitendo hivyo.
‘Mimi ni binadamu,Kama binadamu yeyote naumia sana ninavyonyanyapaliwa,’alisema Barasa.
Anasema kwenye masuala ya urembo hayuko nyuma ana mawigi 15 na zaidi ya pea za viatu virefu ‘High hills’30.
‘Napenda sana urembo na pia naandika kitabu cha maisha yangu kiitwacho
"Dream Boy"ambacho kitaeleza historia nzima ya maisha yangu na jina la
albanu yangua ya injili inaitwa "Bora Siku"alisema Barasa.
‘Namtumikia Mungu na natumaini Mungu anakubali utumishi wangu,’alimalizia Barasa.