London, England. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amemtaka
mchezaji wake kipenzi cha mashabiki Juan Mata kujifunza kukaba ili
kujihakikishia namba katika kikosi chake.
Kiungo huyo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa
klabu hiyo wa mwaka kwa misimu miwili iliyopita, lakini tangu Mourinho
ametua hapo amepoteza nafasi yake ndani ya Stamford Bridge.
“Sababu ya kwa nini kwa sasa hapati nafasi ya
kucheza sana ni mambo nitakayozungumza naye si kuongea hadharani,”
alisema Mreno huyo.
“Alicheza dhidi ya Everton tangu mwanzo wa mchezo
na unaweza kuangalia uchezaji wake. Na aliingia akitokea benchi dhidi ya
Basel wakati timu inaongoza bao 1-0 ... kipi kikubwa alichokifanya.
“Kitu kilichonifanya kumchezesha Ramires na Oscar
karibu na wapinzani na Mata akiwa namba 10 nyuma ya mshambuliaji ili
aweze kupitisha pasi za mwisho na kwa sababu najua ana kipaji kikubwa,”
alisema Mourinho.
“Lakini kitu kingine ni lazima mchezaji azoee jinsi tunavyocheza.”
Chelsea walifungwa 1-0 na Everton katika ligi wiki
iliyopita kabla ya kuchapwa 2-1 nyumbani na Basel ya Uswisi katika
mchezo wa ufunguzi wa Kundi E katika Ligi ya Mabingwa pale Jumatano.
Mata alikuwa kiungo tegemeo wa klabu hiyo msimu
uliopita, lakini Mourinho ameonekana kupenda kumtumia zaidi Oscar kama
kiungo mshambuliaji.
“Nataka kumfanya Oscar kuwa namba 10,” alisema kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, Inter Milan na Porto.
“Nataka wachezaji wengine...kujifunza namna ya kucheza na vile walivyozoea kabla.
“Kama kuna mtu yeyote ataniambia Oscar hatokuwa
mchezaji bora wa Chelsea msimu huu nitampiga vikali. Nataka
kuwathibitishia mashabiki kwamba mimi ni bora