"NITAZAA KUZAA MFULULIZO" DAVINA
STAA wa filamu hapa Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka juu ya azma yake ya kuzaa mfululizo kabla mtoto wake mdogo aliyemzaa miezi kadhaa iliyopita hajakua kiivyo.
Akizungumza na kinasa sauti cha Stori 3, Davina alisema sababu za kufunguka hayo ni kutokana na kuona anapaswa kuzaa haraka mtoto wa pili ili amalizane na biashara ya kulea na ajikite zaidi kwenye uigizaji.
“Unajua nimeona kuwa kulea siyo kitu cha muda mchache hivyo unatakiwa umalize kwanza ndiyo uendelee na kazi zako ambapo nimeona ni bora nitafute mwingine harakaharaka ndipo nijikite katika filamu,” alisema Davina
CREDIT : GPL