Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya ameendelea kumshutumu mkurugenzi wa Global Publishers Erick Shigongo kwa kumchafua na kuahidi siku moja kuongea na kuweka wazi na ushahidi kila kitu kati yake na Shigongo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram @irenewaferegola8, uwoya ameandika:
“Ipo siku ntaongea ukweli kuhusu shigongo na ushaid pia ntatoa…usilo lijua nikama usiku wagiza ndomana atawadanganya wasio na akili na wasio mjua….ntapgana nae mpaka tone la mwisho la damu yangu ntasema kila kitu kwanin ananichukia…na ntaweka kila kitu waz….den wenye akili watajua naongea nin…simuogop atakama atanichafua kiasi gan…hizo kwangu ni matone yamvua bado mvua yenyewe…I don care kwaatakae muamin but mwisho wa siku ukweli utaonekana na atataman ardhi ipasuke……mim irene uwoya sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa nahaaidi ya kwamba ntaongea kila kitu btwn me n him….eeh mwenyez ? MUNGU nisaidie. “
Shutuma hizi zimekuja baada ya gazeti la Risasi linalomilikiwa na Global Publishers katika ukurasa wake wa mbele Jumamosi iliyopita kuandika habari yenye kichwa cha habari ‘UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU’, na baadaye Irene alipost Instagram picha ya gazeti hilo na kuandika:
“Minimti wenye matunda milele siogop kupigwa mawe…shigongo kamua kunichafua coz nakes nae mahakaman…anadhan ntaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho wasiku sheria iatafata mkondo wake….minayake mengi nayajua ila ngoja ninyamaze nisimwagiwe tindikali”