Hili ni tukio la kusikitisha, lakini lenye mafunzo kibao ndani yake....
Tukio hilo lilitoke mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu ndani ya kanisa la Pentekoste la nchini Kenya ambapo wanandoa wawili walikuwa wakila kiapo cha maisha mbele ya mchungaji wa kanisa hilo....
Dakika chache kabla ya wanandoa hao kuapishwa na kuruhusiwa kuvishana pete, Mchungaji wa kanisa hilo aliwauliza waumini kama kuna yeyote mwenye pingamizi la kufungwa kwa ndoa ya wapenzi hao...
Baada ya swali hilo, mwanamke mmoja alisimama na kuelekea mbele ya kanisa hilo huku akiwa na vyeti mkononi....
Alipomkaribia mchungaji, mwanamke huyo alipaaza sauti yake na kusema kuwa ndoa hiyo haistahili kufungwa kwa sababu yeye na bwana harusi wanamtoto waliyemzaa pamoja na kwamba walikuwa na mipango ya kuoana....
Kilichoendelea baada ya hapo ni VITUKO.