Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana
na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya
Machui, alipofika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
kumpa pole, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika
Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk
Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio
hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi
chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali
ya tindikali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza
Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya
Machui, akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na
watu wasiojulikana, Mjini Unguja, Zanzibar alipofika katika Hospitali ya
Muhimbili kumpa pole, ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu. Dk Nchimbi
alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo
watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi
chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali
ya tindikali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto)
akimuhakikishia Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani
Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar jinsi wizara yake itakavyopambana
kwa kuwakamata wale wote watakaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa
kutimia kemikali ya tindikali. Dk Nchimbi alifika hospitalini. Dk
Nchimbi alifika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa
pole padri huyo ambaye anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya
kupata matibabu zaidi. Hata hivyo, Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo
akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali
itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na
vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikaliPicha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.