WAKATI kukiwa na utapeli mwingi katika mitandao ya kijamii sehemu
mbalimbali duniani, Bara la Afrika imelezwa kuwa kinara wa utapeli huo
kwenye mitandao hiyo ya kijamii.
Geofrey Hilmary ni kati ya wadau wakubwa wa mitandao ya kijamii aliyeamua kuanika sura za wadada hawa akidai
kwamba ni kati ya sura hatari kwa utapeli, Watu mbalimbali hususan watu
maarufu ndani na nje ya nchi wamewahi kukumbwa na utapeli wa aina
hiyo,matapeli wengi hutumia picha za uongo huku wengine wakitumia picha
za wasichana warembo.
Mbali na picha hizi zilizowekwa kwenye mtandao wa Facebook na Geofrey Hilmary kuwa zinatumika kwa utapeli, Habarimpya.com pia
iliwai kufanya utafiti na kubaini aina ya utapeli pamoja na nchi
wanazotoka baadhi ya mapeli hao, Utafiti huo ulibaini mambo mbalimbali
pamoja na njia wanazotumia mtapeli hao wa mitandaoni matapeli wengi
hutoka katika nchi za Senegal na Nigeria,Kenya na Tanzania, matapeli
wengi kutoka Senegal wanatumia njia za kuomba akaunti ya benki ili
wakutumie pesa.
Katika maelezo yao hupenda kutumia majina na picha za wasichana
warembo huku wakidai kwamba wao ni yatima na wanalelewa katika vituo vya
watoto yatima baada ya wazazi wao kuuawa katika mapigano na vurugu za
kisiasa.
Katika maelezo yao matapeli hao humtaka mtapeliwa kutuma tarifa
zake zote kuanzia majina yake matatu kazi yake mtaa anaotokana na namba
ya nyumba pamoja na namba ya akaunti ya benki huku wakidai kwamba
wazazi wao walikufa na kuacha pesa nyingi benki lakini kutokana na
kwamba wao ni yatima hawaruhusiwi kufuatilia pesa hizo.
Wanakwenda mbali zaidi na kumtamanisha mtapeliwa kwamba akisha tuma
taarifa zake pesa hizo zitahamishwa kutoka kwenye akaunti ya wazazi wake
na kuingia kwenye akaunti ya mtapeliwa na kisha mtapeliwa atashugulikia
paspoti na viza ya mtapeli huyo kisha wataambatana pamoja katika maisha
ya raha mstarehe.
Njia ya pili ya utapeli wa kwenye mitandao ni ile inayotumiwa
na Wanigeria, wanigeria wao wanajia mbili za utapeli moja ikiwa ni
kukutaka ununue vitu kama vile magari nyumba ama kukutafutia nafasi ya
kazi katika nchi za ulaya, ikiwa sababa na kukutafutia visa ya kwenda
kuishi katika nchi hizo.
Nchini Kenya matapeli wengi wa mitandao wanatumia nafasi ya
kumdanganya mtapeliwa kwamba watamtafutia nafasi za masomo nje ya nchi
hivyo unachotakiwa kufanya ni kujaza fomu maalum wanayokutumia na kwamba
utalipia fomu hiyo kati ya dola za kimarekani 100 hadi 150 lakini
gharama zingine za masomo watalipa wao na baada ya hapo watakusaidia
kupata kazi katika nchi za Ulaya na Marekani, kisha wataanza kukata
asilimia 10 kwenye mshahara wako kwa miaka mitano.
Endelea kuwa nasi, kesho
tutakuletea njia za utapeli zinazotumiwa na watanzania, kwani hili la
watanzania ni bab kubwa kuliko vyote na ndiyo njia inayowanasa watu
wengi hususan wakina dada