Mtu mmoja mkazi wa manispaa ya
Morogoro amefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kutokea mlipuko katika
tenki la lori la mafuta ya Petroli wakati akifanya matengenezo katika
kituo cha mafuta cha Simba oil cha mjini Morogoro.
ITV imeshuhudia jitihada za jeshi la polisi na
kikosi cha zimamoto na uokoaji wakishirikiana na wananchi katika kuondoa
mwili wa marehemu ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda
wamesema marehemu alikuwa akichomelea vyuma ndani ya tenki hilo
lililokuwa limeharibika ambapo gafla ulitokea mlipuko na kupelekea
marehemu kukosa hewa ingawa jitihada za kumtoa akiwa Hai zilishindikana
kutokana na kukosa hewa.
Kwa upande wake mwakilishi wa zamu wa kikosi cha
zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Masoud Ramadhan amesema uchunguzi
wa haraka uliofanyika umebaini kuwa baada ya kutokea mlipuko
uliosababishwa harufu kali ya mafuta ndani ya tank hilo na ambapo
mamehemu alikosa hewa
Mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi
na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa
wa Morogoro.