Takwimu hiyo ilitolewa jana na
Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii, Rosely Kaihula wa Mfuko wa Maendeleo ya Watoto
Ekama, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya mtoto wa kike
duniani itakayoadhimishwa Oktoba 11, mwaka huu.
Mtaalamu huyo alisema sababu zingine
ni mazingira magumu ikiwamo kutokuwa na kipato kwa wazazi ama walezi pindi
mtoto anapohitaji mahitaji muhimu hali inayomsabaisha arubuniwe na hatimaye
kujikuta na ujauzito.
Mratibu wa masuala ya Familia wa
Shirika la SOS Children’s Villages, Magdalena George, alisema lengo la
maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya masuala mbalimbali
yanayomsibu mtoto wa kike, na yataishirikisha serikali, watoto na NGO’s
mbalimbali.
Maadhimisho
ya mwaka huu ambayo yatafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Benjamin Mkapa na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Anna Maembe, yatakuwa na kaulimbiu inayosema: “Chochea
ubunifu kuboresha elimu ya mtoto wa kike.”