Jengo la TTCL lenye ghorofa 12 lililoshika moto katika ghorofa ya sita.
Askari
wa Kikosi cha Zimamoto akijiandaa kuingia ndani ya ofisi za TTCL
zilizoshika moto, hata hivyo kutokana na kuwa na vifaa duni walishindwa
kuingia ndani.
Moto ukiendelea kuwaka katika baadhi ya ofisi.
Magari
ya Kikosi cha Zimamoto kutoka Kampuni ya Altimate yalianza kuwasili kwa
ajili ya kusaidiana na wenzao wa Kikosi cha Zimamoto kutika Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam.
Kituo cha mafuta cha Puma ambacho kipo jirani na jengo la TTCL.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira
ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.
Moto huo ulikuwa unawake katika ghorofa ya sita ya jengo
hilo na ulikuwa unawake katika vyumba vitatu kwa mara moja.
Habari Mseto ilifanikiwa kufika mapema katika jengo hilo na
kukuta pilika nyingi za wafanyakazi kuondoa magari yao, na magari ya shirika
hilo kongwe nchini.
Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha
Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya
wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto
kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini
walifukuzwa kama mbwa,
Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure
na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za
ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.