Hatua
hiyo imechukuliwa baada ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal,
kufanya ziara mkoani Kilimanjaro na kuagiza watu waliofanya hivyo
wakamatwe mara moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema diwani huyo anatuhumiwa kujipatia Sh
milioni 9.6 kwa njia ya udanganyifu.
Wengine
wanaoshikiliwa ni Zakayo Kimathi (52) mkazi wa Mandaka, anayedaiwa
kupokea Sh milioni 10.3, Oforo Kimambo (56) mkazi wa Mandaka anayedaiwa
kupokea Sh milioni 29.
Wengine
wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo kwa njia ya udanganyifu ni Daud
Mallya (69) mkazi wa Chekereni aliyepokea Sh milioni 8.6, Richard Mlaki
(69) mkazi wa Kiboroloni alipokea Sh milioni 18.6 na Focus Herman (88)
mkazi wa Kilototoni aliyepokea Sh milioni 36.
Boaz
alisema kwa sasa watuhumiwa watatu hawajapatikana. Alieleza kuwa pamoja
na watuhumiwa hao, polisi imemkamata Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandaka
Monono, Hassan Nduva (41) na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Vendelini
Shayo (58) kwa kuhusika kufanikisha malipo hayo.
Dk
Bilal alitoa agizo hilo mapema wiki hii wakati akizindua vituo vya
kupozea na kusambaza umeme maeneo ya Kiyungi, YMCA na Makuyuni.
Alipokea
taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuwapo kwa wananchi ambao hawakulipwa fidia
zao, kutokana na kuwapo watu waliotumia ujanja wa kupokea fedha hizo, Sh
milioni 169.2.
“Halmashauri
ya Moshi Vijijini ndio ilikuwa wakala wa malipo hayo na ndio iliyofanya
tathmini kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji, ambapo wao walipeleka
tathmini hiyo kwa Shirika la Umeme (Tanesco), ambalo lilitoa fedha hizo
hivyo Tanesco hawahusiki,” alisema,” alisema Boaz.
-Habari leo
-Habari leo