Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu
nchini
UVUMI
uliozagaa juu ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi mstaafu
Omary Mahita kuwa ni mgonjwa na amepooza upande mmoja si za kweli.Juhudi za kumtafuta na
kuzungumza naye nyumbani kwake eneo la Forest kata ya Boma Manispaa ya Morogoro
ambapo alishangazwa na uvumi huo na kusema kuwa hiyo ni mara ya pili kwa yeye kuvumishiwa
hivyo.
IGP mstaafu huyo ambaye amestaafu mwaka
2006, akizungumza na mwananshi wa habari hizi nyumba kwake alisema kuwa amekuwa
akishangazwa na watu wanaomvumishia kuwa yeye ni mgonjwa na amepooza jambo
ambalo si sahihi.
“Nakumbuka mwaka 2006 nilivumishiwa kuwa naumwa
sana, jambo la kushangaza mimi nilikuwa Arusha kikazi kwenye mambo ya TANAPA
nikawa napigiwa simu ya kupewa pole nashangaa, sasa hii ni mara ya pili
nimepigiwa sana simu za kupewa pole, sijui nani anavumisha hivyi,” alisema Mahita.
Akizungumzia maisha yake ya sasa Mahita alisema kuwa
kwa sasa ajishughulisha na kilimo katika eneo la Dakawa wilayani Mvomero
na amekuwa akilima mazao ya Mpunga, Mahindi na Alizeti.
Alipoulizwa juu ya kuwa na wazo la kugombea nafasi
yeyote katika vyama vya siasa aliendelea kukana kuwa hana mpango wa kugombea
nafasi yeyote, na kama uvumi huo unatokana na hisia hizo hao wanaofanya hivyo
wajipotezea muda.