Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.
Duru zinasema kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.
Mnamo siku ya Jumanne waziri mkuu Zeidan alitoa wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kukomesha vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini Libya.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo