Marehemu enzi za uhai wake.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, kaka wa marehemu Nassoro
Ally, alidai kuwa alipata taarifa ya kuugua kwa dada yake kabla hajafa
kutoka kwa majirani wa marehemu waliomuambia kuwa dada yake anaumwa
kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa mtu mmoja (jina
linahifadhiwa) na hawezi kutembea, hivyo wakamuomba aende kumuona.Aliendelea kudai kuwa baada ya kwenda nyumbani kwa dada yake huyo alimkuta ndani akiwa hajiwezi na alipomuuliza kinachomsumbua alimficha.
“Nafikiri alikuwa muoga kusema alichofanyiwa na huyo mtu japokuwa majirani walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa dada yangu alipigwa mateke,” alidai Ally.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo alirudi ndani na kumbeba mgongoni dada yake huyo ambaye alikuwa hawezi kutembea mpaka kwa balozi wa nyumba kumi kwa ajili ya kutoa maelezo.
“Baada ya kutoka kwa balozi Rahma alianza kutoka damu nyingi sehemu za siri na muda mfupi baadaye akawa amekata roho, hivyo tukafanya utaratibu wa kuutoa ule mwili pale kisha kesho yake tukamzika,” alisema.
Mwandishi wetu alipofika katika eneo la tukio hakuona kaburi la mtoto ila aliona la mama yake tu, hivyo inadaiwa kuwa Rahma alizikwa bila kutolewa kiumbe kilichokuwa tumboni, kitu ambacho ni kinyume cha taratibu za kibinadamu.
Afisa mmoja wa polisi mkoa wa Tanga wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema wanaendelea na uchunguzi.