MSANII wa Bongo Movie, Devota Mbaga hivi karibuni alipatwa na kisanga
cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong
Kong, nchini China kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara.
Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa kitendo hicho cha kuvuliwa nguo
zote na maofisa wa uhamiaji mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa amebeba ‘unga’.
Akizungumza na
mwandishi wetu kwa njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa,
alishikwa sehemu zake za siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji.
“Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye
kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote
ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko.
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi
hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kama
hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa alikotoka.
“Kwa kweli
nimeumia sana kwa kitendo nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima
na kila nikikumbuka naumia,” alisema Devota.