Search in This Blog

MSHINDI WA "BIBI BOMBA" AMBAYE AMEJIONDOKEA NA KITITA CHA SHILLINGI MILIONI 12

Bi.Mgeni Ibrahimu (katikati) akiwa na wadhamini wa shindano la Bibi Bomba kutoka kampuni ya ‘Wazazi Nipendeni’ iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii’
Baadhi ya top 5 ya Bibi Bomba kabla ya kupatikana mshindi.
Mtangazaji (katikati) Babu wa Kitaa akiongea na Bi.Mgeni kabla ya kutangazwa mshindi, kulia ni Bi.Velonica Kayombo
Bi.Mgeni akifanya manjonjo yake mara baada ya kutangazwa mshindi.
 
MASHINDANO ya kumtafuta Bibi Bomba yalimalizika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Complex uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na mwanamama Mgeni Ibrahimu kuibuka kidedea.
Kwa kuibuka mshindi, Mgeni alijinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi milioni 12 zilizotolewa na Clouds Media Group ambao ndiyo walikuwa waandaaji.
Katika shindano hilo lililohudhuriwa na mke wa Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, aliyemwakilisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Veronica Kayombo alitwaa nafasi ya pili na kuondoka na shilingi milioni 5 huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Thabiza Tungalaja aliyeondoka na kitita cha shilingi milioni 3.
Licha ya kuwazawadia washindi hao watatu wa kwanza, pia washiriki wengine watano waliosalia nao walipewa vyeti na kampuni hiyo kama utambuzi wa ushiriki wao katika shindano hilo la Bibi Bomba Season 2.
Akiongea na Clouds Tv, mshindi wa kwanza, Mgeni alisema amefurahia sana kupokea kwa ushindi huo kwani hakutegemea.

“Nafurahia sana kushinda, nimepokea kwa furaha ushindi huu, sikutegemea kabisa kwani mchakato ulikuwa mgumu,” alisema Mgeni.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger