MUME wa staa wa sinema za Kibongo, Gadner Dibibi amemchimba biti
mkewe mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ kwenda kujirusha na
mashosti zake bila kuongozana naye.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Jack alisema mumewe hamzuii kwenda kujirusha
viwanja lakini anachotaka ni kuona wanaambatana kama kumbikumbi kitu
ambacho kinamweka njia panda kwani marafiki zake huwa wanashindwa
kujiachia pindi wanapokuwa na mumewe huyo.
“Mume wangu amenizuia
kabisa nisitoke peke yangu na hata mashosti zangu wakihitaji kampani
yangu hulazimika kunifata kiwanja nilichopo na mume wangu, sina ujanja
tena nishaolewa miye,” alisema Jack.