HALI
inatisha! Kundi la vijana wahuni lililopo maeneo ya Mgeninani,
Mbagala-Kuu jijini Dar, linadaiwa kuhusika katika vitendo vya kulawiti
wanafunzi wa shule za msingi na chekechea zilizopo maeneo hayo na
kusababisha madenti hao kusema: “Tumechoka kulawitiwa!”
Awali
‘makamanda’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) walipokea taarifa kutoka
kwa mmoja wa wazazi waliolalamikia watoto wao kulawitiwa na vijana hao
na kuwaomba wafike eneo hilo ili kukomesha matukio hayo.
Baada ya
kupata taarifa hizo, timu ya OFM ilitinga maeneo hayo na kuthibitisha
kuwepo kwa matendo hayo ambapo iliwasaidia wazazi hao kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Mbagala-Kizuiani kisha wakapatiwa PF-3 kwa ajili
ya matibabu na uchunguzi wa kitabibu na kuandaa utaratibu wa kuwakamata
watuhumiwa.
Wakizungumza na OFM, wanafunzi hao waliodaiwa kulawitiwa waliwataja watuhumiwa wawili kwa jina mojamoja ambao ni Side na Mudi.
Walidai
kuwa vijana hao huwachukua wakati wa kutoka shuleni na kuwapeleka
kwenye majumba mabovu kisha kuwaingilia kwa zamu huku wakiwachezea
sehemu za siri na kuwapa shilingi mia mbili wakiwaonya kutunza siri.
Wanafunzi
hao ambao wengi wana umri chini ya miaka 15 wa shule ya msingi na
chekechea, waliendelea kutiririka kuwa wamekuwa wakilawitiwa na wanaume
hao kwa takriban miaka miwili na kukiri kuficha siri hiyo kwa kuogopa
kudhuriwa na wahusika.
Miongoni mwa wanafunzi waliofanyiwa unyama
huo ni denti wa darasa la nne (14), mwingine wa chekechea (7), wa darasa
la pili (8) na mtoto mdogo wa kiume (4) ambao wote majina yanahifadhiwa
kwa sababu za kimaadili.
Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa
Shule ya Msingi Maendeleo, Mteghenjwa Kidika ambaye baadhi ya wanafunzi
waliofanyiwa unyama huo ni wa shule anayosimamia, alikiri kuwepo kwa
hali hiyo tete.
Alisema wanafunzi hao walio chini ya darasa la tano
hufanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa hawapatiwi nasaha tofauti na wale wa
darasa la tano hadi la saba wanaopewa elimu hiyo.
Baada ya kufanyiwa
uchunguzi kwa vipimo vya daktari katika Hospitali ya Mbagala-Zakhem, Dar
ilibainika kuwa walikuwa wamepata madhara makubwa sehemu za siri.
OFM
iliweka kambi kwa muda wa siku mbili ikiwa na wazazi na jeshi la polisi
ambapo ilifanikiwa kumnasa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Said na
kufikishwa katika Kituo cha Polisi Kizuiani-Maturubai na kufunguliwa
jalada la kesi namba MB/RB/10209/2013 ULAWITI huku wengine wakiendelea
kusakwa.