Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan.
WAZIRI mkuu wa Libya Ali Zeidan aliyetekwa nyara na watu wenye silaha mapema leo alfajiri kutoka katika hoteli anayoishi mjini Tripoli ameachiwa huru.
Serikali ya Libya imesema kuwa tukio la kutekwa nyara huenda lilikuwa ni
ulipizaji kisasi dhidi ya kitendo cha kikosi cha jeshi la Marekani
mwishoni mwa wiki iliyop
ita ambapo mwanaharakati mmoja anayehusika na
kundi la al-Qaeda alikamatwa katika mitaa ya mji huo mkuu.
Kutekwa nyara kwa Ali Zeidan kunaakisi udhaifu mkubwa katika serikali ya
Libya , ambayo inashikiliwa mateka na wanamgambo , wengi wao wanatoka
katika makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.
Wanamgambo hao wanasemekana kuwa wamekasirishwa na hatua ya jeshi la
Marekani kumkamata mtuhumiwa, anayehusika na kundi la al-Qaeda, ambaye
anafahamika kama Abu Anas al-Libi, na wanaishutumu serikali kwa kuruhusu
kikosi hicho cha Marekani ama kushirikiana nacho kumkamata mtuhumiwa
huyo.
Wavamia hoteli
Watu walioshuhudia wameliambia shirika la habari la Associated Press
kuwa zaidi ya watu 150 waliokuwa na silaha wakiwa katika magari ya pikup
waliizingira hoteli ya Corinthia kabla ya majira ya alfajiri leo.
Kundi kubwa la watu hao liliingia katika jengo hilo la hoteli, baadhi
wakisalia katika eneo la kupokelea wageni wakati wengine walielekea
katika ghorofa ya 21 ambako Zeidan alikuwa akiishi.
Watu hao wenye silaha waliwafunga pingu walinzi wa waziri huyo mkuu
kabla ya kumkamata na kuondoka nae, amesema mtu mmoja aliyeshuhudia
tukio hilo, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina kwasababu ya
kuhofia usalama wake.
Wamesema kuwa Zeidan hakutoa upinzani wowote wakati akiongozwa kuelekea katika magari ya watu hao.
Mtafaruku wa uongozi
Katika ishara ya mtafaruku nchini Libya , kukamatwa kwa Zeidan
kumeelezwa na duru mbali mbali kuwa ama ni kuwekwa kizuwizini, ama ni
utekaji nyara, unaoakisi jinsi wanamgambo wanavyoingiliana na mfumo wa
uongozi ambao hauko pamoja nchini Libya.
Mohamed Shaaban , meneja wa usalama katika hoteli hiyo ya Corinthia,
amesema kuwa watu hao wenye silaha wameuonyesha uongozi wa hoteli hiyo
waranti wa kukamatwa kwa waziri mkuu huyo , ambao wamedai umetolewa na
mwendesha mashtaka mkuu wa serikali.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali imesema haijatoa waranti kwa kukamatwa Zeidan.
Kiongozi wa zamani wa Libya marehemu Muammar Gaddafi
Wakati polisi na jeshi la nchi hiyo hayako katika hali nzuri, wanamgambo
huorodheshwa kutumika kama walinzi wa usalama katika mashirika ya
serikali , licha ya kuwa utiifu wao uko kwa makamanda wao badala ya
maafisa wa serikali na mara kadha wameweza kuwatisha maafisa.
Wanamgambo
wanatokana na vikosi ambavyo vimepigana katika vuguvugu la kuuangusha
utawala wa kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011, na mara kadha
wanatambulika kama "wanamapinduzi".
Lakini hivi punde mbunge katika bunge la Libya amesema kuwa waziri mkuu
huyo ameachwa huru na wanamgambo waliomteka leo alfajiri. DW.