AANGUKIA KICHWA NA KUFARIKI DUNIA WAKATI AKIPANDA DALADALA HUKO ILAL BOMA JIJINI DAR
Mtu mmoja
ambaye jina lake bado halijafahamika, amefariki dunia baada ya kuteleza na
kuanguka wakati alipokua akijaribu kudandia Daladala maeneo ya Ilala Boma,
Jijini Dar es Salaam, asubuhi leo. Marehemu huyo baada ya kuanguka na kupiga kichwa
kwenye lami, alipasuka kichwa na kuvuja damu nyingi kichwani, na kufariki
katika eneo la tukio.