HANDAKI LA WAZUNGU LATUMIKA KUWATESA WATOTO NA KUWALAWITI HUKO MABWEPANDE
Zaidi ya watoto 60
wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa
Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna
jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa
kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao
hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.
Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa
la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam
na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni
hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.
Watoto hao walitekwa na Wazungu w
awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan
ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika
Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao
walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.
Walisem a w atoto hao
wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na
kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao
hubakwa na kulawitiwa.
"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki,
tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika
mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.
"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa
kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa
moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme
tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na
machozi.
Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka
huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na
Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi
wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.
"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na
watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka,
nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.
"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu
nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu,
wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na
kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa
wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel
Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na
mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja
ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili
awatoroshe.
"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani
mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani
eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari
limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.
"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui
tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na
njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa
tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.
"Tulikula saa 10 jioni, wali na
maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa
kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.
"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli,
alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka
na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na
kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza
vizuri," alisema Emmanuel.
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema
baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni
hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus
(29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d
a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi
mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.
"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na
kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku
akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.
Alisema zaidi ya watoto saba walipotea
katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine
wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa
uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei
alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es
Salaam.
Alisema makachero wa polisi wamewahoji
watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka
watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.