Mrembo
na msanii mpya kwenye kiwanda cha bongo movie aliyefahamika kwa jina la Witness
Mmbando “19|” ametoa onyo kali kwa msanii Jackline Wolper awe makini kwa nafasi anayoishiikilia ya
ustaa kwani siku si nyingi atapinduliwa na nafasi yake kuchukuliwa na mrembo
huyo mwenye umri mdogo na sifa kibao za kuigiza zaidi ya Wolper.
Habari
zilizopatikana mwishoni mwa juma zilisema kuwa Witness ambae ni kabila moja na
Jackline Wolper na amekuwa na jazba na Wolper kutokana na msanii huyo kushindwa
kuwasaidia wasanii wanaotoka sehemu moja na yeye.
Akiongea
na Mdadisi Mambo Blog, mrembo huyo mwenye elimu ya juu ya Computer alianza kumchana Wolper
kwa mambo anayoyafanya huku akisema wasanii wa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha
jinsi gani wanavyo mchukia “ Unajua Wolper anajisahau sana ameshindwa kuwainua
wasanii wachanga wa mkoa wake na kuna wakati mwingine akipigiwa simu anawakatia
na kuwajibu vibaya halia ambayo inawakera sana ikizingatia kuwa yeye ndiye mtu
wa kuwasaidia kuinua vipaji vyao” Alisema Witness ambae pia ni mtoto wa kigogo
wa polisi nchini
Witness
aliongeza kusema Wolper alitakiwa hata siku moja kuwatembelea wasanii wa mkoa
wake japo kwa kuwapa moyo lakini wapi hata siku moja hajawahi kuitisha hata
kikao nao japo kuzungumza nao, hali hiyo imepelea wasanii hao kukosa matumaini
na Wolper ambapo anasema sio lazima awapatie pesa la hasha ushauri na maawazo
mazuri tu yangetosha.
Mrembo
huyo ambae ameonesha kipaji cha hali juu kwenye filamu ya NGEMA ambayo siku za
hivi karibuni itakuwa mtaani huku Mzee Magari nae akimtabiria makubwa kwenye
ulimwengu wa sanaa kutokana na kipaji chake pamoja na muonekano wake “Huyu
binti kwanza umbo lake na uso vinaendana na uigizaji hawa ndio wasanii
tunahitaji ili kuzalisha mastaa wengine baada ya sisi kustaafu hivyo Witness
namtabiria baraka kwenye tsania hiyo natoa angalizo kwa mastaa wa kike waliopoa
sasa kukaa mkao wa kula la sivyo watapotezwa vibaya” Alisema