Search in This Blog

MAALIM GURUMO AUGUA GHAFLA, ALAZWA MUHIMBILI, HII NI BAADA YA KUPATA SHINIKIZO LA DAMU


GWIJI wamuziki wa dansi, Muhidin Maalim Gurumo ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Gurumo, Juma Mbizo na Said Mdoe, waliokuwepo Muhimbili, wameuambia mtandao huu kuwa mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo.
Wamesema kwa sasa haliyake inaendelea vizuri na amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 1.
Wajumbe hao wamesema siku chache zilizopita, Gurumo alikuwa kwenye afya njema na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati hiyo kilicho fanyika Vijana Social Hall Kinondoni.
Aidha, wajumbe hao wamedai kuwa kwamujibu wa mke wa Gurumo, Bi Pili, ni kwamba hata jan amwimbaji huy oalikuwa hana tatizo lolote na alifanya mizunguko yake bila y amikwaruzo yoyote.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Gurumo, Bi Asha Baraka amewataka wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali ya mwanamuziki huyo aliyeitumikia fanik wamiaka 53, inaendelea vizuri.
Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger