UKAMILIFU wa binadamu ni pale anapozikwa, kabla ya hapo si kamili!
Jumanne Rashid (24), Jumatatu iliyopita aliamka nyumbani kwake, Manzese
Dar akiwa mzima wa afya na kuelekea kazini Kiwanda cha Urafiki Plastic
Co. Ltd kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Lakini ghafla, ukamilifu wake uliyeyuka baada ya mashine moja ya kiwanda hicho kumkata mkono wote wa kushoto na kuanguka.
Aidha,
aliulalamikia uongozi huo kwamba waliuchukua mkono wake bila
kuwashirikisha ndugu zake, wakauzika kienyeji jirani na kiwanda chao,
tena bila kumfahamisha yeye mwenye mkono.
Jumatano iliyopita, raia waliuona mkono huo na kulazimika kuwaita
Polisi wa Kituo cha Urafiki-Ubungo, Dar ambao walipofika, majirani
waliwatuhumu Wachina hao ambao ni mabosi wa Jumanne, kuhusika na tukio
hilo kwani walikuwa na taarifa za kijana huyo kukatika mkono.
Baada ya kuufukua mkono huo, polisi walikwenda kumkamata mwekezaji
anayemiliki kiwanda hicho cha kutengeneza mifuko ya plastiki aitwaye Lee
Slimy na kumhusisha na tukio hilo.
Jumatano iliyopita, Risasi Jumamosi lilipompata Jumanne katika wadi
na. 12 katika Jengo la Kibasila, Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar
es Salaam aliongeza zaidi:
“Siku ya tukio niliingia kazini kama kawaida na kuendelea na majukumu
yangu, baadaye nikabaini tatizo katika moja ya mashine za kiwanda
ambayo ilikuwa imezimwa kutokana na kukatika kwa umeme.
“
Nikaingiza mkono wa kushoto ndani ya mashine hiyo ili kurekebisha
tatizo, lakini ghafla nikashtuka kuona umeme umewaka na mfanyakazi
mwenzangu mmoja (hakumtaja) akawasha ile mashine na kilisababisha mkono
wangu kukatika hapo hapo.”
Jumanne alisema baada ya tukio hilo alikimbizwa Hospitali ya Palestina, Sinza, Dar kabla ya kuhamishiwa Muhimbili.
“Iliniuma
sana, niliuacha mkono wangu ndani ya mashine nikawa sijui ulipo. Hakuna
bosi aliyekuja kuchangia gharama za matibabu. Nashangaa kusikia leo
(Jumatano iliyopita) mkono wangu umeonekana ukiwa umezikwa,” alisema kwa
masikitiko Jumanne mkazi wa Manzese, Dar.
Risasi Jumamosi
juzi lilimtafuta kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Komba ili azungumzie suala hilo lakini bila mafanikio. Risasi
linaendelea kuchimba.