Stori: Imelda Mtema
MTOTO Seleman Rajabu (16) ambaye mguu wake ulianza kuvimba wenyewe tangu alipozaliwa, amechangiwa fedha zaidi ya Sh. Mil. 4 ambazo zimemwezesha kwenda nchini India kupata matibabu.
Akizungumza na mwandishi wetu, kijana huyo alisema hana chochote cha kuwalipa Watanzania waliojitolea kumsaidia, bali atawaombea kwa Mungu ili awabariki kwani maumivu ya mguu wake yanampa mateso makubwa.
“Nawashukuru sana wote walionichangia kwa moyo wao wa huruma na kuona ni jinsi gani ninateseka kila siku, nitazidi kuwaombea kwa Mungu wazidi kufanikiwa zaidi,” alisema Sele.
Zaidi aliishukuru Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa kuendesha kampeni ya kumchangia kupitia magazeti yake ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa kwani kupitia magazeti hayo, Watanzania wengi waliweza kuguswa na tatizo lake na kujitolea kumchangia.
Seleman hakusita pia kumpongeza mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Runinga ya Channel Ten, Hoyce Temu kwa kumpa fursa ya kumuonyesha katika kipindi chake ambacho pia kimetoa fursa ya watu kumchangia.
“Namshukuru sana dada Hoyce Temu na Mungu azidi kumbariki maana kipindi chake pia kimenisaidia sana msaada wa kuniwezesha kuanza kupata matibabu,” alisema.
Akizungumzia safari hiyo ya India, mtoto huyo alisema kila kitu kinakwenda vizuri, tayari ameshaanza taratibu za kukatiwa viza ambapo anatarajia kuanza safari wiki ijayo.
Seleman alianza kuugua tangu azaliwe, mguu ulianza kuvimba taratibu, ukaendelea kukua pasipo kujulikana sababu ambapo mwishoni alipelekwa katika Hospitali ya CCBRT, jijini Dar ambao walishauri mguu huo ukatwe, mama yake akakataa na kuitisha harambee ya kuchangiwa.
-GPL