Search in This Blog

NDOA YA CATHY HATIHATI KUVUNJIKA



IKIWA imebakiza siku moja tu kabla ya kufungwa kwa ndoa ya msanii mkongwe wa tasnia ya filamu, Sabrina Rupia ‘Cathy, mtu asiyefahamika alimtumia ujumbe mumewe mtarajiwa, Salim Rupia wa kumtaka asimuoe mwigizaji huyo kwani wasingedumu.

Akizungumza na kona hii, Cathy ambaye alijinyakulia umaarufu mkubwa kupitia maigizo ndani ya Kundi la Nyota Ansemble, alisema tangu wakiwa katika harakati za uchumba mwaka 2002, baadhi ya watu walionekana kutokuwa na imani kabisa na ndoa hiyo jambo ambalo lilimkosesha amani zaidi baada ya kukaziwa zaidi siku moja kabla ya harusi.
“Ulikuwa mtihani mkubwa sana maishani mwangu, nilimuomba sana Mungu, nashukuru aliweza kuitikia maombi yangu.
“Iliposalia siku moja tufunge ndoa, uliingia ujumbe kwenye simu ya mume wangu ukimtaka aachane kabisa na mpango wa kufunga ndoa na mimi kwani isingedumu hata kidogo,” alisema Cathy.

Hata hivyo, Cath alifanikiwa kuolewa na kwa sasa ndoa yao imetimiza miaka kumi na mbili huku wakiwa wamejaliwa watoto watatu.
“Kila ndoa yangu ilipokuwa ikitimiza mwaka mmoja nilikuwa nikiwataarifu wote walioitabiria mabaya,” alisema Cathy.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger